Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akifuatilia Mahubiri yaliyotolewa na Padre Paul Haule wa Kanisa la Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam. |
Akiwa
mwenye afya njema na furaha Mama Magufuli aliyekuwa pamoja na Mke wa
Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wamesali ibada ya asubuhi katika kanisa
hilo na baadaye kusalimiana na waumini nje ya kanisa.
Baada ya kumalizika kwa Ibada, baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo wameelezea furaha yao ya kumuona Muumini mwenzao akiungana nao katika ibada na wamemuombea afya njema.
"Nimejisikia furaha sana kumuona Mama Magufuli amekuja Kanisani akiwa na afya njema na uso wa bashasha, na ninamuombea kwa Mungu aendelee kumsimamia" amesema Mama Mabula.
"Nimeshukuru sana kumuona Mama yangu Mama Magufuli, Mwanajumuiya mwenzangu leo Kanisani, huku afya yake ikiwa imetengemaa zaidi, tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu na tunamuombea aendelee kumpigania afya yake izidi kuwa imara" amesema Thomas Simon.
"Kwa kweli siku ya leo kwangu mimi ninafuraha sana kwa kumuona Mama
akiwa kanisani, na zaidi Mama wote wawili kwa sababu pia amekuja Mke wa
Mhe. Waziri Mkuu, kwa hiyo kwetu sisi ni furaha sana kama Parokia,
tunafurahi sana tunaposhirikiana na viongozi wetu" ameongeza Epifania
Ngonyani.
Mwezi uliopita Mama Janeth Magufuli aliugua na kulazwa katika wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alipata matibabu kwa siku mbili na kisha kuruhusiwa.
source EATV
Baada ya kumalizika kwa Ibada, baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo wameelezea furaha yao ya kumuona Muumini mwenzao akiungana nao katika ibada na wamemuombea afya njema.
"Nimejisikia furaha sana kumuona Mama Magufuli amekuja Kanisani akiwa na afya njema na uso wa bashasha, na ninamuombea kwa Mungu aendelee kumsimamia" amesema Mama Mabula.
"Nimeshukuru sana kumuona Mama yangu Mama Magufuli, Mwanajumuiya mwenzangu leo Kanisani, huku afya yake ikiwa imetengemaa zaidi, tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu na tunamuombea aendelee kumpigania afya yake izidi kuwa imara" amesema Thomas Simon.
Mwezi uliopita Mama Janeth Magufuli aliugua na kulazwa katika wodi ya Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alipata matibabu kwa siku mbili na kisha kuruhusiwa.
source EATV
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon