YAKO MATUNDA MENGI LIKO MOJA KWA FAMILIA

Katika jamii za kitanzania ziko aina tofauti tofauti za familia na kila familia ina msingi wake na hasa misingi ya ndoa zilizonyingi ni katika imani, kama sio ukristo utakuwa uislamu au imani katika mabibi au mfumo wa wa kiukoo. katika makala hii fupi sana nitajitahidi kuonyesha jinsi ambavyo tunaweza kuwa na familia tunazosema  ziko katika ndoa ingawa kiuhalisia hakuna msingi wa imani yoyote ndani ya ndoa husika.

FAMILIA KAMA TUNDA LA NDOA
Familia yoyote ile tawi la ndoa, tunaposema kuwa ni tawi la ndoa maana yake ndoa ni shina la familia,kwa maana nyingine hakuna ndoa hakuna familia, pia imani ni mzizi wa ndoa hivyo tunaweza kusema ."imani ikikosekana hakuna ndoa na kama hakuna ndoa hakuna familia"lengo la makala hii sio kuzungumzia ndoa ila ni kuzungumzia zao la ndoa yaani familia, familia nyingi za kitanzania zimekuwa ni familia zisiso na msaada au mchango kwa taifa kwasababu wengi ambao wamepewa kuwajibika na familia zao wamekuwa ni watu ambao hawana uwezo na utayari katika kuwalea na kusimamia familia katika maadili yanayotakiwa. taifa limekuwa na ongezeko kubwa la watu waliokosa maadili ni kwasababu familia zimeshindwa kusimamiwa na wale waliopewa dhamana ya kuzisimsimamia, mume na mke katika ndo wana wajibika sana kuhakikisha familia zao zinalindwa.

YAKO MATUNDA MENGI LIKO MOJA KWA FAMILIA 
Hapa nitoe muhutasari mfupi tu, kuwa familia ni chemchemi ya mafanikio katika taifa pasipokuwa na familia makini zenye hofu ya Mungu ni rahisi sana kuwa na taifa la wasomi wengi wasiokuwa na uadilifu, kama familia zinakosa uadilifu hatuhitaji kulalamika wapi tumejikwaa kama taifa tulipokwamia ni pale tunapoona kuwa swala la uadilifu kwa familia, utovu wa nidhamu katika taifa unaoonekana leo ni zao la wazazi ambao hawakuona umuhimu wa kuwalea watoto wao katika maadili stahiki,tunahitaji familia yenye matunda yafuatayo:-haki,amani,furaha,upendo,tumaini,imani,heshima,uadilifu,nk hatuwezi kupata yote haya ikiwa familia nyingi zinapita katika sintofahamu 
 "familia bora ni zao la baba na mama mwaminifu"
Ev.isack e
+255 757 324 092
Unity of changes programs Tz(UCPT) 
facebook page, unity of changes programs
 
Latest
Previous
Next Post »