SALAMU ZA KRISIMASI NA MWAKA MPYA 2017 KUTOKA KWA MWL.ABEL MOLLA

MWL.Abel Molla
Hizi ni salamu zangu katika kipindi hiki cha Krismasi na mwaka mpya kwako wewe rafiki yangu na mdau unayenifuatilia kila siku katika mafundisho, huduma, na mambo mengine.
Bwana Yesu asifiwe!
Ni imani yangu kwa neema ya Mungu unaendelea vyema, hata katika changamoto nyingi lakini bado mkono wa Mungu upo pamoja nawe na ukiendelea kusonga mbele.
Rafiki yangu tunapoelekea mwisho wa mwaka huu wa 2016, ninaomba kukushirikisha mambo machache ya msingi sana ya kufanya katika kipindi hicho kwa ajili ya mstakabali wa maisha yako ya kiroho na kimwili pia.
Jambo la kwanza: JENGA UTARATIBU WA KUFANYA TATHMINI YA YA MAISHA YAKO YA KIROHO NA KIMWILI TANGU JANUARY MPAKA DECEMBER.
Jambo hili ni muhimu sana kwa mtu yeyote yule anayetaka kuona mabadiliko katika maisha yake kila siku. Jambo hili likifanya vizuri linaweza kufanya mambo yafuatayo;
# Tathmini itakuonyesha mahali ulipofanya vizuri (mafanikio) kwa kipindi chote cha mwaka mzima katika mipango yako ya mwaka mzima.
# Tathmini itakuonyesha mahali haukuweza kufanya vizuri (failure) katika mipango yako ya mwaka mzima.
# Tathmini itakuonyesha changamoto ulizokutana nazo wakati wote wa mwaka mzima.
Na mengine mengi ila kwa hayo machache yatakupa mtaji wa kufikiri mengine mengi.
FAIDA ZA KUFANYA TATHMINI
# Tathmini itakusaidia kupendekeza njia mbadala wa kufanya jambo tofauti na ulizozitumia wakati uliopita kama ulizozitumia wakati uliopita hazikuleta matokeo yaliyotegemewa.
# Tathmini itakuinulia msukumo ndani yako ya kuongeza bidii katika kutenda jambo unalolitenda ili kupata matokeo yaliyokusudiwa.
# Tathmini itakusaidia kukutengenezea mazingira mapya ya kiutendaji kwa mwaka unaofuata.
Zipo na nyingine nyingi kwa hizo chache Mungu akupe kufikiri zaidi na kuweka kwenye matendo.
.....KIPINDI KIJACHO TUTAENDELEA NA JAMBO LINGINE......
By. Mwl. Abel Molla.
Kwa maoni, ushauri na maswali,
0763438164 au 0713418104
abelmolla200@gmail.com
WhatsApp: 0763438164.
Previous
Next Post »