IFAHAMU HISTORIA FUPI YA KANISA LA AFRICAN INLAND CHURCH TANZANIA(AICT)

Leo katika Historia ya kanisa la AICT lilikotoka kabla ya kuwa hivi lilivyo:Mnamo mwaka 1877-1909 lilikuwa likiitwa CMS yaani Church Missionary Society lilianza kazi ya kuhubiri Injili katika Afrika Mashariki,Bagamoyo Tanganyika,mwezi Julai 1876.Mwaka 1909-1937 Peter Cameron Scott alianzisha AFRICA INLAND MISSION (AIM)mjini Philadelphia,USA.Madhumuni yake ilikuwa ni kuhubiri Injili na kuanzisha makanisa katika bara la Afrika.Mwaka 1937-1956 kanisa kuanzishwa rasmi na kupewa jina la EKLEZIA EVANJELI YA KRISTO (E.E.K) nakupewa katiba iliyo wapa mamlaka na kanuni tatu zilizo andikwa katika katiba; 1.Kujitawala lenyewe 2.Kujitegemea lenyewe 3.Kujieneza lenyewe.Wakati huu katiba ilikuwa imeandikwa kwa lugha ya Kisukuma na miniti zote za vikao. viliandikwa kwa Lugha hii.1957 Jina la kanisa EKLEZIA EVANJELU YA KRISTO lilibadirishwa na kuitwa AFRICA INLAND CHURCH TANGANYIKA Jina hili jipya liliandikwa katika katiba.Kujitawala halisi kwa A.I.C.Tanganyika kulipatikana 12/2/1960 katika mkutano wa Synod na Field Council.Kwa wakati huo mkuu wa kanisa alikuwa akiitwa DIRECTOR yaani Mkurugenzi.Mkurugenzi wa kwanza AICT ni Mch Jeremia Mahalu Kisula ambae baadae ndie aliyekuwa Askofu wa kwanza wa kanisa hili.Jina la Ukurugenzi lilibadirishwa na kuitwa Uaskofu mnamo mwaka 1966 na kuweza kuchaguliwa kila baaada ya miaka minne.Baadhi ya Majina ya viongozi wa kanisa hili tangu mwanzo.1.Oneil .Luten Shergold 2.Mch Alexander mckay.


SOURCE;Makongoro kwaya FB
Previous
Next Post »

3 comments

Write comments