NINI HASA MWELEKEO WA MUZIKI WA INJILI TANZANIA?



By isack,e
Ndugu msomaji wa blog hii naomba uungane na mimi kupata majibu ya maswali ambayo yanauumiza sana moyo wangu. Katika tasnia ya muziki wa injili kwakweli tumeweza kupiga hatua ukilinganisha na miaka mitano iliyopita.lakini jambo ambalo nataka ujaribu kulitazama kwa undani hasa kwanini muziki wainjili hapa nchini haukui kwa kiwango kinachotakiwa?.katika maendeleo ambayo nayaona kwakweli muziki wetu umeendelea ni katika eneo la muimbaji mmojammoja,lakini ukweli ni kwamba wasanii wa muziki hapa nchini pamoja na uwezo mkubwa walionao katika kutunga mashairi mazuri katika nyimbo hizo tatizo kubwa liko katika swala la live show ambambo wasanii wetu wengi wanaimba kutumia play back jambo ambalo halileti radha nzuri katika uimbaji.

Ziko bendi zinazofanya vizuri kama next level,grolious worship celebration na wasanii wengine binafsi kama john lisu,pastor safari na Minza Nkila ambao kwa kweli wako katika mstali wa mbele katika kuimba live show lakini pia bila kusahau kwaya kama AIC chang’ombe (cvc) na kinondoni revival choir kwakweli tunaona jitihada zao katika eneo zima la live show.

Yapo makundi mbalimbali ambayo tumeshuhudia yakija vizuri sana kwenye eneo la live performance lakini kitambo tu yanafifia au yanameguka vipande vipande hii ni hatari sana kwa eneo la uimbaji.mara nyingi sana nimekuwa ni kivutiwa na muziki wa south Africa ambapo unakuta kwamba kuna bendi ambazo zinaimba kwa kutumia live show pia waimbaji binafsi kama Zaza,solly mahlangu na Rebecca malope unawezakuona kabisa kwamba ingawa wanaimba kwa lugha za kwao lakini kunamvuto Fulani wa kiroho unaoweza kumpa hamasa msikilizaji kujua nini kinaimbwa.
solly mahlang akishambulia jukwaa(picha msaada wa mtandao)

Tatizo kubwa ambalo ninaona katika muziki wetu wa injili ni swala zima la ubinafsi na tama ya pesa ambayo kwakweli kabisa mpaka tuvuke kwenye hii sehemu hapo ndipo waabuduo halisi wataweza kupatikana,kwa taarifa mablimbali kutoka katika makanisa na huduma mbalimbali unakuta msanii wandani(nchini) anapoalikwa anataka kwanza pesa nyingi sana jambo ambalo kweli pesa inahitajika ili huduma iendelee lakini sio vizuri kutangulizam kwanza pesa badala ya huduma. Naomba niweze kuwapongeza wasanii kama upendo nkone na Cosmus chidumule ni wasanii ambao kwakweli wakotayari kutanguliza huduma kwanza badala ya pesa na maombi yangu Mungu aweze kuwainua zaidi.

Katika swala la kupiga hatua kwa Muziki wa injili lazima waimbaji wa muziki huu wasijione kuwa ni wasanii wa nyimbo za injili,ila waimbaji wa muziki wa injili wapate kuutafuta zaidi uso wa Mungu na kufanya kama huduma kamili katika mwili wa kristo tukito usanii tutakuwa tayari katika tasnia ya muziki wa watu wanaomwabudu Mungu kwa roho na kweli. Hebu na wewe jiulize tatizo ni nini? pia mwelekeo wake ni upi?
Previous
Next Post »