Bishop sylvester Gamanywa |
ZIJUE TOFAUTI KATI YA "KUNYAKULIWA
KANISA" NA "YESU KURUDI MARA YA PILI"
Unyakuo na kurudi mara ya pili ni matukio mawili tofauti japokuwa yote ni matukio ya siku za mwisho na yote yanamlenga Yesu mwenyewe. Kuna utata katika kupambanua baadhi ya maandiko kama yana maana ya unyakuo au Yesu kurudi mara ya pili dunia.
Tukio la Unyakuo ni wakati Yesu Kristo anakuja kulichukua kanisa kutoka duniani kwenda mbinguni kama ilivyoandikwa katika (1 Thes 4:13-18; 1 Kor. 15:50-54.) Waliokufa katika Kristo watafufuliwa na tulio hai tuliosalia tutabadilishwa miili na kunyakuliwa ili kumlaki Bwana mawinguni. Kwa maelezo mengi unyakuo unalenga kanisa tu. Lakini wakati wa Yesu kurudi mara ya pili duniani, walengwa ni taifa la Israeli na hukumu dhidi ya mataifa yatakuwepo duniani kwa wakati huo, kufuta uovu na kusimika utawala wa milenia duniani (Rev.19:11-16; )
1. Wakati wa unyakuo watakatifu (kanisa) tunakutana na Bwana mawinguni (1 Thes.4:17). Wakati Yesu anaporudi mara ya pili duniani anakuja pamoja na watakatifu wake (kanisa) (Ufu. 19:14).
2. Wakati tukio la unyakuo Litafanyika kabla ya dhiki kuu (1 Thes.5:9; Ufu. 3:10). Tukio la Yesu kurudi mara ya pili duniani litafanyika baada ya dhiki kuu (Ufu 6-19)
3. Tukio la unyakuo linafanyika kuwaepusha watakatifu (kanisa) na dhiki kuu (1 Thes. 4:13-17, 5:9). Wakati Yesu kurudi kwake mara ya pili duniani ni kwa ajili ya kuwaokoa wayahudi na kuyahukumu mataifa yote yaliyokuwa upande wa Mpingakristo (Mat.24:40-41).
4. Tukio la unyakuo litakuwa ghafla na siri (1 Kor. 15:50-54). Wakati Yesu atakaporudi mara ya pili duniani kila jicho litamwona (Ufu. 1:7; Mat. 24:29-30).
5. Kurudi kwa Yesu duniani mara ya pili ni tukio litakalofanyika baada ya matukio kadhaa yaliyotabiriwa kufanyika katika siku za mwisho (2 Thes. 2:4; Mat.24:15-30; Ufu. 6–18). Lakini unyakuo ni tukio linalotarajiwa kufanyika wakati wowote kuanzia hivi sasa (Tit.2:13; 1 Thes. 4:13-18; 1 Kor. 15:50-54).
HATARI YA KUAMINI KANISA
LITAKUWEPO DUNIANI WAKATI WA DHIKI
1. Madai ya kwamba kanisa litakuwepo duniani kwenye dhiki kuu yanakinzana na agizo la Yesu la kuhubiri Injili kwa kila kiumbe ili aaminiye na kubatizwa ataokoka na asiyeamini atahukumiwa (MK.16:16) Kwa maana katika kuamini injili mtu anapata ahadi ya uzima wa milele ambayo kilele chake ni kuingia mbinguni; na asiyeamini anakuwa chini ya hukumu ya milele kwenda jehanamu ya milele
2. Madai ya kwamba kanisa litakuwepo duniani kwenye dhiki kuu mpaka mwisho yanakinzana na Ahadi ya Yesu Kristo kwa wanafunzi wake kuwa kaenda kuwaandalia mahali mbinguni na kisha "atarudi tena kuwachukua" ili alipo yeye mbinguni na wao wawepo pamoja naye (YH.14:1-3;1 Thes.4:17).
3. Madai ya kwamba kanisa litakuwepo duniani kwenye dhiki kuu mpaka mwisho yabatilisha unabii kwa kanisa kukusanyika mbele ya Kiti cha hukumu cha Kristo kwa ajili ya kupokea thawabu na taji za utukufu kwa ajili ya utumishi wao katik Kristo walioufanya wakiwa hai duniani.( 2Kor.5:10)
4. Madai ya kwamba kanisa litakuwepo duniani wakati wote wa dhiki kuu yanamfanya Mungu akiuke neno lake la kutokuwahukumu wenyehaki na waovu pamoja. (1 Thes.1:10; Ufu.3:10) Dhiki kuu ni hukumu ya Mungu ya kuifanya Israeli imkubali Masihi waliyemkataa (Yer.30:7) na kisha kuyahukumu mataifa yaliyokubali chapa ya mpingakristo wakati wa dhiki kuu. (Mt.25:32-34)
5. Madai ya kwamba kanisa litakuwepo duniani wakati wa dhiki kuu kunadhoofisha imani ya kujikana nafsi na kuishi maisha ya utakatifu duniani. Maana faraja ni matumaini ya kuingia mbinguni; “Kisha sisi tulio hai tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. Basi farijianeni kwa maneno hayo. (1 Thes.4:17-18)
Tukutane kwenye sehemu ya nne. Kama umeguswa na mada nisaidie kwa ku-like post hii na kisha uwarushie na marafiki zako. Ubarikiwe sana.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon