Ev.Isack e |
Maombi yangu ya wazi kwa watu wote,binafsi nakushukuru Mungu kwa uaminifu na upendo wako wa ajabu sana kwangu,yako mengi umefanya umenipa kujua zaidi kuwa upo na ni halisi,machozi nimetoa ya kutosha,lakini bado ukasema wewe utabaki kuwa Mungu.nimejitahidi kufanya mazuri mengi nikifikiri ndio tiketi ya kusogea lakini ukasema hapana. Mungu wangu unanipenda umeniambia "mwanangu kuwa mnyenyekevu kwanza"hapo ndipo nimegundua kuwa mazuri yanakuja sio kwasababu nimetenda mema ila kwasababu nimenyenyekea.
Mungu nakuomba uende na mimi,mwaka 2016 uwe mwisho kwangu kutembea nisaidie nikimbie sitaki kutembea nipe nguvu nipe uweza nifanye kwa kiwango kikubwa,2017 nataka nikuone Baba anza na mimi umalize na mimi. Sitaki kufa bila kumaliza kusudi uliloweka ndani yangu nisaidie nitimize.
Mungu naomba enda na wasiokujua,wako wengi hawajajua uzuri wako na ukuu wako wewe umesema hupendezwi na kifo cha mwenye dhambi,baba waokoe wakujue wewe tusipungue ila tukaongezeke. Haya nimaombi yangu katika Jina lako Bwana,amen
Ev.Isack, e
2016
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon