EV.Isack e |
Kusudi
la somo hili ni:- kuruhusu nuru ya Mungu ipate kutawala
katika maisha yetu na tusiteswe tena na Maradhi ,uhitaji na magumu ya kila
namna katika maisha yetu ya kila siku.
Utangulizi;
Mazingira ya kawaida
tunayoishi asili yake ni rohoni, hakuna jambo ambalo linaweza thibitika katika
mwili pasipo kuanzia rohoni,kwa maana hiyo hakuna njia yoyote ambayo
unawezakuiishi kesho kabla leo haijawa dhahiri, soma 2kor 4:18. Maandiko yanasema hivi “tusiviangalie VINAVYOONEKANA.kwa maana
vinavyoonekana ni vya muda tu; bali VISIVYOONEKANA ni vya milele”. Kila kitu unachokiona katika mazingira
unayoishi uwe na uhakika kina asiri ya rohoni. Pia Yesu aliwatahadharisha
wanafunzi wake katika mathayo 6:25 inasema “..Kwasababu
hiyo nawaambieni,msisumbukie maisha Yenu,mle nini au mnywe; nini wala miili
yenu mvae nini,maisha je si zaidi ya chakula,na mwili zaidi ya mavazi?”. Kwa
ufupi alikuwa anawaambia kwamba wanauwezo wa kuishi maisha ya ushindi na
mafanikio katika mazingira waliyokuwa wanaishi.
Mafundisho,
Ndugu natamani sana
uweze kutambua umuhimu wa kuathiri ulimwengu wa roho,unaweza kujua namna ya
kuathiri ulimwengu wa roho usipojua
umuhimu wake iko shida katika hilo eneo. Nitaonesha pointi nne ambazo
zitatusaidia kujua umuhimu wa kuathiri mazingira tunayoishi
1 .unapoathiri
mazingira unapewa maarifa na ujuzi wa
kuyatawala mazingira mazingira hayo Daniel 1:17 inasema basi kwa habari ya hao vijana wanne,
Mungu aliwapa maarifa na ujuzi katika elimu na hekima; Daniel naye alikuwa na
ufahamu katika maono yote na ndoto.soma mwanzo1:26
2 .Unapoathiri Mazingira Unapata Kibali Cha Kusimama Mbele Ya Wakuu Daniel
1:20 kunauwezekano mkubwa sana kuwa na maarifa mara kumi zaidi. Hapa utagundua
kuwa kuna uwezekano mkubwa sana wa kuwa mtawala mahali ambapo watu wanaweza
sema huwezi. Hawa vijana wanne tunaosoma kwenye Daniel wasingeweza kutambua
uwezo walio nao inawezekana hata hiki kitabu cha Daniel kisingekuwepo ila
kitendo cha kukubali kufanya mabadiliko katika mazingira yao kunatoa fursa ya
kuwa sehemu ya utawa katika ufalme wa Nebkadneza.
3. unapoathiri mazingira unapata nafasi ya kuwasiliana na Mungu bila kujali
mazingira ya nje daniel 2:17-19 mfalme nebukadreza alipotaka kuwauwa wenye
hekima wote hawa vijana walikuwa na ujasiri wakuweza kusogea mbele za Mungu na
kuweza kuathiri mazingira hatimaye wakapata tafasiri sahihi ya ndoto.
Yakobo
5:17,18, 1falme 17 & 18 unapoathiri mazingira unaweza kuamuru mbigu
zikabadili majira ya mvua. Tunaweza kuona mfano wa eliya
yeye kutokana na uovu uliokuwa umezidi katika taifa la Israel aliweza
kusimamisha majira mpaka pale taifa litakapogundua dhambi yake na kutubu. Tunaona
uwezo wa Eliya kuita mvua nayo ikatii.
4. kuathiri mazingira kunaruhusu kujua/kufunuliwa mambo yaliyojificha
yaliyo sirini Daniel 2:22 inasema yeye hufunua mambo ya fumbo na ya
siri;huyajua yaliyogizani, na nuru hukaa kwake.kupitia athari
inayoletwa na maombi huweza kuathiri mazingira na kujua siri na fumbo za Mungu,
Mungu anaweza kukufunulia kitu ambacho kimedumu kwa muda mrefu bila majibu hapo
mtaani kwako.
Hitimisho.
Katika mambo yote ni
muhimu kutambua kuwa mazingira yako yanatawaliwa na utakatifu yaani vazi
jeupe,ufunuo 22:14,tunaweza kuvaa hili vazi kwa namna moja nayo ni kumpokea Yesu
kuwa Mwokozi wa maisha Yohan 1:12,ndugu yangu nakuomba tutamani kupokea karama
ya Mungu ambayo ni uzima wa milele.
Kumbuka kuwa ili
kumkaribia Mungu inahitaji mahusiano mazuri na Mungu wala si vinginevyo
“….IKO
NGUVU KATIKA NENO…”
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon