Kutembea katika neema ya Yesu (walking with the grace of Jesus ).effeso 2:8-9



Na,Isack,e simu 0717 307 056

Utangulizi
Tunapozungumza neema maana rahisi kabisa ni upendeleo wa kupata kitu au jambo Fulani ambalo
hukustahili kupata.mfano:- kupata upendeleo wa marks darasani,au kupata mshahara tofauti na wenzako ambao mko daraja moja,au kumilikishwa kitu cha thamani ambacho kwakawaida usingeweza kuwanacho.
Katika lugha ya kiingereza kwa mujibu wa free media dictionary ameeleza kwa kiingereza kuwa “grace is the state of being protected or sanctified by the favor of God”. Hivyo kwa namna nyingine neema ni hali ya kulindwa au kuokolewa kutoka dhambini kwa upendeleo wa Mungu.
Hivyo tunaposema kutembea katika neema ya Mungu inamaana ni kutembea au kuenenda kwa upendeleo na si vinginevyo,tofautisha neema na rehema,rehema ni msamaha unaoweza kupewa na mtu uliyemkosea. Bwana Yesu asifiwe sana.
Tunaishi tunavyoishi na tunatenda tunayotenda sio kwa sababu tunajua sana au tunauwezo mkubwa sana wa kufanikisha mambo yanayotuzunguka, hapana upo mkono usioonekana kwa macho ya nyama unaotuwezesha kuwa hivi tulivyo sio kwa ujanjaujanja wako.

Mafundisho
Ukiangalia katika maandiko asili ya mtu halisi aliyeumbwa na Mungu sio kuishi maisha ya kushindwa au kupata shida ni mtu ambaye aliumbwa kwa mfano halisi wa Mungu soma mwanzo 1:26,ili kumiliki na kutawala,lakini baadae tunaona mwanadamu huyohuyo anaanza kutembea katika mwanvuli unaitwa neema kwanini?.Tunatembea katika neema kutokana na sababu zifuatazo ambazo moja imesababishwa na Mwanadamu,nyingine imesababishwa na Mungu mwenyewe:-
1. Kwa sababu tumetenda dhambi
rumi 3:23 “sote tumetenda dhambi na hiyo dhambi ilifanyika zamani sana,hivyo kitendo cha kuwepo neema ni kwasababu dhambi ilichukua haki yetu/uwezo wetu wa kumiliki adui aliuchukua.
hivyo hakukuwa na sheria yoyote ya kushindana na dhambi, hata leo yamkini umejitahidi sana kuacha dhambi ukifikiri kwamba labda unaweza kwa nguvu zako au kwa akili zako,kwa kujitahidi huwezi hii ni kwa sababu ya dhambi  soma rumi 5:20,gal 3:19.ina maana kwamba kabla ya dhambi hakukuwa na sheria na sheria hiyo ilikuja ikiwa bado ni plani ya Mungu kumwondoa mwanadamu katika dhambi,na hivyo kwa kutilia mkazo sheria hiyo alikuja kristo ili kuikamilisha. lakini kupitia kristo tunaona neema inapatikana,rumi 5:17 hallelujah.
2. kwa sababu ya upendo wa Mungu mwenyewe
Neema ni upendo kamili wa Mungu hakuna namna unaweza kuchomoka katika mtego wa adui pasipokuwepo upendo,upendo una huruma ndani yake,upendo unaagano ndani yake, upendo,upendo unakupa kumiliki,upendo unaruhusu kibali yoh 3:16-17.
 Hivyo upendo unatupa kupata neema kwasababu:-
                                    i. neema ni ahadi ya imani kupitia kristo gal 3:19-12
                                    ii. neema inatupa kibali cha kuwa warithi pamoja na kristo gal 3:28,29
ni neema pekee inayowezesha mimi na wewe kuishi hivyo tunavyoishi wala sio kwa sababa  tunamjua sana Mungu pia masomo yako,maisha yako future yako inategemea sana neema ya Mungu ili kufikia pale ambapo Mungu anakuwa amekusudia.
Hitimisho
Kumbuka hukuja na kitu chochote hapa duniani ulikuja wewe ukiwa umebeba kusudi la Mungu tu na kwa kufanya hivyo Mungu haangalii kitu kingine anaangalia neno lake alilolitamka kabla hujazaliwa ili lipate kutimia.jitoe kwa Bwana kama dhabihu uone mambo ambayo Mungu atakufanyia .soma rumi 12:1,2
BWANA YESU AKUBARIKI SANA
Previous
Next Post »