isack,edward |
SEHEMU YA KWANZA
Kwa kuanza naomba nitoe maana ya vazi. vazi ni aina fulani ya nguo ambayo hutumika kumsitiri mtu au mwanadamu.Vazi huwa na uwezo wa kumfanya mtu aonekane kwa namna nadhifu au isiyo nadhifu.katika sehemu hii ya kwa nza nitaangalia zaidi vazi kwa namna ya kibinadamu yaani ya kawaida. Kama tunavyo fahamu .
Tanzania kama nchi lazima iwe na vazi la rohoni na vazi la mwilini,najua ni sehemu ngumu lakini naomba nielezee jambo lililonishitua sana katika kikao cha bunge maalum la katiba hasa pale Mbunge wangu wa ubungo Bwana john mnyika alipokuja na marekebisho katika rasimu ya kanuni za bunge hili,ambapo pamoja na mambo mengine aliyojadili mbunge huyu amekuja na hoja ya kutaka vazi la shati la kitenge liruhusiwe kuvaliwe katika Bunge hili. kilicho nishtua sana kuliko yote ni kuona kuwa asilimia kubwa ya wabunge wameonekana sana kutetea suti na tai.huu nauita mtazamo wa kimaghalibi,jambo ambalo ni hatari sana kwa taifa linalotaka kutunza utamaduni wake ,swali la kujiuliza ikiwa wawakilishi wetu ambao tunaamin wanaelewa umuhimu wa mtanzania wanakuwa hawana mtazamo mzuri katika swala la utamaduni maana yake hii ni nini sasa?.
vazi la taifa ni muhimu sana kwa taifa lolote maana huo ndio utambulisho wa haraka zaidi kwa taifa lolote lile.ikiwa kwenye chombo cha muhimu sana katika nchi bunge maalum la katiba ambalo lipo kwa muda mfupi tu kunakuwa hakuna makubaliano kuhusu vazi la taifa ina maana kwamba utambulisho wetu katika nchi umepigwa teke.
jambo kama hili linapotoke a uwe na uhakika kwamba nchi haina watu ambao wana thamini na kuutambua umuhimu wa kutunza tamaduni zao.sio kwamba napigia debe vazi la kitenge kama mbunge wangu alivyopendekeza hapana ila ninachozungumzia ni nchi kuwa na utamaduni unaoeleweka.ukiona hivi hii ndio hali halisi ya watanzania tuli hatuko makini sana katika kuutunza utamaduni wetu.zipo tamaduni ambazo ni mbaya hazitakiwi kutunzwa lakini kwa tamaduni zinazotunza heshima ya nchi lazima zitunzwe na kythaminiwa kuliko kitu chochote kile.
katika kuhitimisha sehemu hii wewe mtanzania ambaye huone umuhimu wa kuwa na vazi la taifa lazima ufunguke katika hiyo sehemu na kuona uthamani wake.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon