change of thought |
katika mambo yote ni kumshukuru Mungu kwa Mambo makubwa aliyofanya katika mwaka huu 2013. Pamoja na shukurani hizi zote lazima kuna alama ambazo tumekuwanazo katka mwaka 2013, nilazima kuanzia katika alama hizo ndipo tunaweza kuutazama mwaka unaokuja kwanamna ya ndani zaidi.Najaribu kuliangalia jambo hili kwa level ya kitaifa,yapo mabadiliko mbalimbali yametokea katika nchi yetu Tanzania ni kunifanya niyaone kama alama katika ustawi wa nchi. mambo hayo ni haya yafuatayo:-
mdororo katika ustawi wa jamii,
kama ni mtu unayefuatilia kwa ukaribu mambo malimbli yanayohusu nchi yetu utakubari kuwa jamii ya mtanzania katika huu mwaka imejikuta katika hali ngumu sana,hasa katika eneo la kipato na hata mahitaji muhimu ya kijamii kama afya na elimu,katika elimu tumeshuhudia kuna danadana za kila aina ambazo hatuwezi kuona adhali za moja kwa moja lakini kitambo tu zitaonekana. sio kwamba nalalamikia serikari kuu lakini ukweli ni kwamba katika eneo la mstakabari wa elimu katika nchi yetu katika mwaka 2013 imekosa mtu wa kuisemea kwa usahihi badala yake tumepokea na kusikia malalamiko kuanzia serikalini mpaka mwananchi wa ngazi ya chini kabisa. kwa maana hiyo kuwa na ustawi mzuri katika nchi lazima wawepo watu ambao watasema kile ambacho kitaleta mabadiliko. pia katika swala la afya bado kumekuwa na mdororo katika sector ya afya pamoja na jitihada mbalimbali tumeona zikifanyika ili kunusuru uhai wa mtanzania lakini ukweli nikwamba vifo na matibabu hafifu vimekuwa janga katika mwaka 2013.
hali ngumu ya uchumi na mabadiliko ya hali ya nchi .
katika eneo jingine hali ya uchumi kwa maana ya kipato cha mtu mmoja mmoja kimekuwa hatari katika mwaka 2013 jambo linalosababisha kuongezeka kwa makali ya maisha kutokana na ongezeko kubwa la gharama, lakini ni vigumu kuelezea swala uchumi pasipo kuhusisha na mabadiliko ya nchi ambayo yamesababibsha ukame kwa baadhi ya maeneo kupelekea shughuli za uchumi zinazohusisha kilimo kushindwa kufikia malengo yaliyokuwa yamewekwa. pia swala la migogoro ya wafugaji na wakulima ni alama ambayo tuningia nayo mwaka 2014 bila kupatia suluhu.haya mambo yote yanelezea namna gani uchumi wa mtanzania haukuwa wa kuimarika katika mwaka 2013. lakini jambo ambalo ni kubwa sana katika eneo la uchumi ambalo tunaondoka nalo kama alama ni pale ambapo tumepoke ahadi nyingi sana kama nchi katika eneo la uchumi,ziko ahadi za marekani,china japani na nchi nyingine nyingi kuhusu mpango wa kuimarishwa kwa uchumi wa nchi yetu. hii naiona kama alama kwa maana kuna hayo mabadiliko tuliyoyaona katika ahadi hizo ambayo yameifanya nchi mbali na kuwa na marafiki lakini kuna maadui ambao wamezaliwa kutokana na ahadi hizo. hivyo kwa waombaji wanoomba kwa habari ya nchi hakikisha unakaa vizuri katika maombi ili Mungu aifanikishe mipango mizuri ya nchi hii.
katika kuukaribisha mwaka 2014 ,
Kuelekea mwaka mpya,katika jambo ambalo watu wengi sana
wanaferi katika maisha ni kukosa mipango,ukiwa na mipango inakusaidia kujua
hatua unazoendea.mwaka huu unaisha lakini ninauhakika kabisa ndugu hukuwa na
mipango mwaka huu kama ilikuwepo ni ile mipango ya kila siku mfano kumjua
Mungu,kupiga hatua za maisha na vitu vingine vingi ambavyo ni general
sana.mipango ninayoizungumzia hapa ni ile mipango ya miaka 20 ijayo na namna
unavyoweza kuitimiza kila mwaka
Nakutakia heri ya mwaka mpya na mafanikio mema ukiutafakari ukuu wa Mungu yeye aliyekupa kibali cha kuwa hai mpaka sasa kwa maana anataka akutumie kwa wakati huu. kaza viwango katika kmtafuta Bwana ili akija akukute umejipanga.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon