pima kazi uliyopewa na Bwana



IBADA YA KUWAAGA WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE UBUNGO MORDERN SECONDARY SCHOOL
29 september 2013
Kupima kazi uliyopewa na Mungu
Somo;gal 6:3,4,7-9
Na Isack Edward,simu 0717307056,e-mail edwardbujiku@ymail.com blog http//eibujiku.blogspot.com
MR ISACK,E
Kusudi:tupate kutambua kuwa sisi kama mawakili wa siri za Mungu tunawajibika kuona kuwa yale yote ambayo mungu ametupa kufanya basi yanafanyika kwa usahihi.
Utangulizi
Kipimo ni alama inayo weza kuonesha ufanisi wa kazi ambayo mtu anakuwa ameifanya kama imefikia kiwango au bado haijafikia,kiwango cha kazi uliyoifanya unapimwa na wewe mwenyewe na si vinginevyo gal 6:4.jina la Bwana libarikiwe.
Mwanadamu ameumbwa kwa kusudi kubwa moja tu ambalo ni kumtumikia Mungu,Hapa inamaana ya kumtumikia Mungu katika Roho,maandiko yanasema katika wagalatia 5:16… basi nasema,enendeni kwa Roho wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Pia yohana 4:24 inasema Mungu ni Roho,nao wamwabuduo imewapasa kumwabudu ndani ya/katika roho na kweli. Kwamaana hiyo kama Mungu ni roho basi kazi zake zinafanyika katika roho na si kwingineko yaani haya ambayo tunayafanya leo tayari yameshafanyika katika roho leo ni hitimisho la kile kilichokwisha kufanyika. Haleliyah?soma 2kor 4:18. Tumeitwa kumtumikia mungu tangu tumboni mwa mama zetu soma galatia1:15,yeremia 1:4,5
Katika somo hili nitajaribu kukutizamisha vipengele mbalimbali vinavyohusu wajibu wako kama mkristo.
Mafundisho
(i)                 tambua kuwa unanawajibika kutumikia kazi/shauri la bwana
Katika kumtumikia Mungu lazima utambue kuwa wewe unawajibika na utawajibika siku ya mwisho Galatia 6:5 maana kila mtuatalichukua fulushi lake mwenyewe,hakuna mtu atakayeweza kukusaisia.kwa maana nyingine hakuna mahali unapoweza kujitetea kwamba hukufanya kazi ya mungu kwa sababu Fulani hiyo haipo.ili kupima uwajibikaji wako lazima kunamatokeo ambayo yataonekana kupitia wewe. Wazazi na wawalezi pamoja na wanafunzi mliopo hapa mnahakika kwamba kazi  aliyowapa Mungu meeitimiza?.

(ii)               Unawajibika kuwasaidia wengine
 Kati ya vitu vya muhimu kabisa ni kuweza kuchukuliana/kusaidiana katika utumishi,wako watu ambao wamekuwa kiimani au wamefikia hatua Fulani ya imani.lazima kuhakikisha kuwa wale ambao ni dhaifu wanasaidiwa kupitia wao.soma gal 6:1-2.haiwezekani unaona watu au mwenzako anaanguka halafu nafurahi hiyo haitakiwi ,lazima uwalejeze kwa bwana .Haleluya watu wa Mungu.

(iii)             Tambua kuwa hautendi kazi ya Mungu kwa mwili bali katika roho
Katika utangulizi tuliweza kutazama eneo hili lakini nakukumbusha tu kuwa unapofanya kiazi ya Mungu kumbuka hili usisahau,unatumika katika roho.kwa lugha nyingine unapanda kwa njia ya roho na si vinginevyo
Leo form 4 wanahitimu sijui nikwakiwango gani wamejiandaa,lakini maandiko yanasema ……yeye apandaye kwa mwili atavuna uharibifu apandaye kwa roho atavuna uzima wa milele. Kile tulichopanda ndio tutegemee kuvuna .Mahusiano yako na Mungu ndio yanayokupa fursa ya kufanikiwa au kutokufanikiwa,. Tutaomba kwa ajili ya form 4 hapa lakini kama umepanda katika mwili wewe tarajia uharibifu, ukivumilia lazima kuna wakati utavuna .gal 6:8-9.

(iv)              Dhambi inatufanya tusitimize mapenzi ya Mungu
rum 3:23 inasema kwasababu wote wametenda DHAMBI,na kupungukiwa na UTUKUFU wa Mungu,dhambi inapunguza utukufu wa Mungu ndani yetu.rum 10:3 inasema kwamaana hawaiju HAKI YA MUNGU,na wakitaka kuithibitisha HAKI YAO wenyewe,hawakujitia chini ya haki ya Mungu.pia rum 1:28 na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao,Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa,wayafanye yasiyo wapasa,ukimkataa Mungu yeye halazimishi anakuacha tu na hasara inakuwa yako wewe wala sio mtu mwingine.

Hitimisho.
Sikia mtu wa Mungu umewekwa hapo ulipo sio kwaajili yako hapana ila ni kwaajili ya kazi ya Mungu naomba ukumbuke hilo.maandiko yanasema bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake yoh 1:12, rumi 10:9 inasema kwa sababu ukimkiri Yesu kwa kinywa chako yakuwa NI BWANA ,na kuamini MOYONI MWAKO yakuwa MUNGU ALIMFUFUA katika wafu UTAOKOKA.10 kwa maana kwa moyo mtu HUAMINI na kupata HAKI,na kinywa hukiri hata kupata WOKOVU. Isaya 55:6-7 MTAFUTENI BWANA maadam anapatikana MWITENI,maadam yu karibu.7 mtu mbaya na aache njia zake na mtu asiyehaki aache mawazo yake.Ndugu saa ni sasa ya kuhakikisha unatenda kazi ya Mungu hakuna Muda wa kupoteza njoo kwa Yesu.


Gal 6:18 Ndugu zangu,neema ya Bwana wetu yesu kristo na iwe na roho zenu. amina
MWISHO 





Previous
Next Post »