KANUNI SABA (7) ZA MWANAFUNZI KIONGOZI
SOMO : 1timotheo 1:12,rumi 8:37
SEHEMU YA PILI
2. Tambua kuwa nafasi ya uongozi haikutofautishi na wanafunzi wengine
Katika mambo ambayo yanaonekana kama changamoto,ni kile kitendo cha mwanaqfunzi anapopewa nafasi ya kiuongozi uwe wa dini au wa shule unakuta anajiweka katika kundi tofauti na wanafunzi wenzake.kitendo hiki kinamadhara makubwa sana kwa kiongozi husika maana itakufanya wewe kuwa peke yako peke yako na wakati mwingine utajiwekea mazingira ya kuchukiwa na wenzako.ni muhimu sana kutokujitofautisha na wanafunzi wenzako.kumbuka kuwa uwanafunzi ndio ulikupa nafasi ya uongozi wala sio uongozi uliokupa uwanafunzi.kuwa makini pia kwenye eneo hili. Hakikisha unaishi maisha ya shule kama mwanafunzi kwa kutii taratibu zilizopo kama wanafunzi wengine tu. Ni muhimu sana kwako kujumuika pamoja na wengine katika majadiliano ya masomo(group discussion) itakufanya kufanana na wanafunzi wengine.
3. matumizi mazuri ya muda.
Soma muhubiri 3:1-8,katika nafasi ya uongozi shuleni kumbuka mambo haya kuwa umepewa saa 24 kama wanafunzi wengine hivyo kitendo chochote cha kupoteza muda ni hasara kwako,hakikisha unamtumikia mungu asilimia mia na unasoma asilimia mia acha kupoteza muda na vitu visivyo vya msingi,pia katika eneo hili la muda hakikisha unapata muda mzuri wa kupumzika,hii itafanya akili yako ipumzike na utakuwa katika nafasi nzuri ya kufauru masomo.kumbuka umepewa masaa 24 lakini sio masaa yote ni ya kusoma hakikisha unakuwa na ratiba nzuri.
4. kujiamini/kuamini unachokifanya
Katika hali ya shule kuna maneno mengi ambayo baadhi yake hujenga hofu miongoni mwa viongozi. Jambo la msingi ni kujiamini kabisa ukiamini kuwa nafasi hiyo uliyonayo umepewa na Mungu hivyo ni lazima kutimiza makusudi ya Mungu bila woga.kitendo cha kutokujiamini kinaweza kukuondoa kwenye maendeleo uliyokuwanayo na kujenga hofu itakayo kuharibia masomo.ili kuondokana nahali hii hakikisha pia kuwa wale wote wanaokupa ushirikiano ndio watakaokuwa pamoja na wewe.
5. Tumia maombi na neno kama silaha yako muhimu
Katika maisha yako kama mwanafunzi na kiongozi ni muhimu sana kwako kutambua kuwa Maombi na neno ni silaha itakayo kuvusha hapo ulipo kwenda hatua nyingine.
Maombi ni hatua au kipimo cha mtu kuzungumza na Mungu katika ulimwengu wa roho ili yale yote yasiyoonekana yapate kudhihirika kwa usahihi. Soma luka 18:1,fillip 4:6 hakuna mafanikio unayoweza kufikia pasipo maombi hakikisha kuwa katika siku zote za maisha swala la maombi linapewa nafasi maana vita vyetu sijuu ya damu na nyama mazingira hayo ndiyo yatakayokupa fursa yakumsikia na kufanya yale tu ambayo Mungu ameyakusudia kwako. Kupitia maombi utajiimalisha katika nafasi uliyopo na hakuna jambo litakalo onekana gumu kwako.
Neno la Mungu ni muhimu sana kwako hakikisha unakuwa na neno la kutosha ndani ya moyo wako ili likusaidie kumtafakari Mungu soma yoshua 1:8,pia neno la Mungu ni hakika yaani limethibitishwa au limehakikishwa kwako hivyo linaweza kufanyika ngao kwako wewe uaminiye angalia mithali 30:5. Pasipo neno la Mungu ni vigumu sana kutimiza mapenzi ya Mungu.
6. Kuwatii wazazi/walezi
Kunachangamoto ambayo huwa ipo kwa wanafunzi wengi hasa pale unapopata nafasi ya uongozi mara nyingine hutaka kushindana na wazazi. Ni kweli kuna wazazi ambao hufanyika kama miiba kwa watoto, lakini ninahakika kwa mtu uliyeokoka ni rahisi sana kutumia hekima na akili tuliyopewa na Mungu ili kutokuwa makwazo kwa wazazi au walezi wetu. Kumtii mzazi maandiko yanasema ndio haki kitendo cha kutokutii mzazi kinawezazuia Baraka ambazo Mungu amekusudia kwako, effe 6:1. Pia kumtii mzazi kunapendeza sana mbele za Mungu soma tena kolosai 3:20, Mungu anataka tuwatii wazazi wetu.
Ikiwa mzazi analeta ugumu hakikikisha maombi yanatumika kama silaha kwako,usishindane na mzazi ila kwakuwa unatambua kuwa Mungu ndiye aliye kuita hakikisha unang’ang’ana mpaka mzazi atambuae wito ambao Mungu amekuitia.
7. kujitoa kwa ajili ya kazi ya Mungu(commitment)
Katika hatua ambayo ni muhimu pia hakikisha kuwa unajitoa kwa kazi ya Mungu asilimia zote,fanya kwabidii ukijua kuwa kuna ujira utakaopokea baada ya kazi hiyo.usimtumikie Mungu kwa mashindano,hauna nafasi ya kushindana na mtu yeyote hakikisha kuwa unatimiza wajibu wako kama kiongozi lakini pia kama mwanafunzi usiruhusu uzembe au ktegea wengine wafanye fanya tu kwa maana Mungu ndiye anayepima utendaji kazi wako wala si mwanadamu,soma kol 3:23 yote yafanyike kwa utukufu wa bwana na si vinginevyo.
HITIMISHO
Ni imani yangu kuwa kuna jambo Mungu anataka ufanye katika nafasi na eneo ulilopo zingatia haya hakika utavuka na kufikia ile mede ya thawabu,fillip 3:12-15.
MUNGU AKUBARIKI
MWISHO
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon