KANUNI SABA (7) ZA MWANAFUNZI
KIONGOZI
SOMO : 1timotheo 1:12,rumi 8:37
KUSUDI: kuwa na hakika kuwa ushindi tulionao ni katika kanuni za kiMungu zinazoongoza maisha yetu.pia kama kiongozi kutambua kuwa ziko kanuni katika kufanikisha mpango wa mungu juu ya maisha yetu.
MAFUNDISHO
Katika mambo mengi yanayowapa shida wanafunzi na wazazi wengi
ni katika eneo la uongozi. Mara nyingi mtoto anapopata nafasi ya uongozi
shuleni huleta shida kwa wazazi hata kwa baadhi ya ndugu. Hofu hii huwa nikweli
maana unakuta wakati mwingine kiwango cha ufauru hushuka nautafiti unapofanyika
unakuta kuna eneo mwanafunzi huyo hakulisimamia kwa usahihi baada ya kuwa
kiongozi. Pia kwa uhakika kabisa utumishi(uongozi) tunaupokea kutoka kwa
Mungu,mith 1:12
Sababu kubwa inayoweza kumfanya mwanafunzi kiongozi asifanye
vizuri ni kutokutambua kanuni sahihi zitakazomfanya kuwa kiongozi bila kuathiri
nafasi yake kama mwanafunzi.
Kanuni hizi zitakusaidia wewe mzazi au mwanafunzi kutambua
hatua madhubuti zitakazo fanya uongozi huo kufanyika Baraka.kanuni hizo ni hizi
zifuatazo;-
1.kujitambua
Katika hatua yoyote ya maisha ya mwanadamu yako mambo/maswali
matano ambayo anatakiwa kujiuliza ili aweze kuishi sawasawa kabisa nampango wa
Mungu. Maana rahisi ya kujitambua ni kuwa na ufahamu wa kutosha kuhusu mfumo
mzima wa maisha binafsi ya mtu Fulani.kujitambua ni muhimu sana maana pasipo kujitambua
huwezi kutimiza wajibu wako kama kiongozi lakini pia kama mwanafunzi.
·
wewe
ni nani(identity)
huwezi kujitambua ikiwa wewe umeshindwa
kujielewa wewe ninani maana kitendo cha kujitambua wewe ninani ni fursa nzuri
ya kukufanya wewe kujua maono uliyonayo.nakama maandiko yasemavyo pasipo
maono watu huacha kujizuia mithali,29:18a,hivyo nafasi ya kujijua kuwa
wewe ninani nifursa nzuri ya kukufanya uwe na utaratibu,kwamaana unajitambua.
Lazima kuwepo kitu kinacho kutambulisha wewe kwa maana nyingine kuishi na
kujitazama wewe kama wewe si wewe kama watu wengine.
·
Asili
yako ni wapi?(source)
Hapa
ndugu unaweza kujitathimini tu kwamba mimi asili yangu ni wapi,nini hasa asili
yangu na ndugu zangu ni wapi.kutambua asili yako kutakufanya uwe na mtazamo
mzuri na ufahamu wa kutosha juu ya wale wanaokuzunguka.hapa nazungumzia kuwa
kwa harakaharaka unafikiri ninani anaweza kubadili ukawaida wa maisha hapo
ulipo.kujua asili yako kutakufanya uwe na mbinu za kuhakikisha unafikia malengo
yote Mungu aliyokusudia kwako. Swala la asili yako pia lazima litazamwe
kimaandiko kwamba umetokana na nini je wewe ni mfano wa Mungu sawa na mwz
1:26?.pia unapotambua asili yako ya kibiblia hautakubali kuwa mstari wa nyuma
maana unajua kuwa asili yako ni Mungu tu.
·
Kusudi(purpose)
Kama
kiongozi lazima utambue kusudi la Mungu kukuweka kwenye hiyo nafasi,au kwanini
upo kwenye hiyo shule,kwenye hilo eneo au kwanini uko kwenye majukumu hayo?
nini hasa Mungu anataka kutoka kwako?. kutambua kusudi ni muhimu sana kuliko
unavyofahamu maana kusudi mimi naweza kufananisha na begi la msafiri,likipotea
inamaana mtu huyo hatavaa wala hataishi kama alivyokuwa amekusudia.kama ambavyo
msafiri huweza kupangilia vitu muhimu katika safari yake ni vema nawewe kutambua
kusudi ulilopewa na Mungu, muhubiri 3:1
·
Thamani
yako(potential)
Kama
mtoto wa Mungu ni mwanafunzi au si mwanafunzi ambaye umepewa nafasi ya kuwa
kiongozi,lazima upate kujiuliza unathamani gani mbele za Mungu?.lakini pia
unathamani gani kwa wanaokuzunguka?.ukijibu haya maswali itakupa nafasi ya
kujiheshimu na kuwaheshimu wengine.soma mwz 39:12 kwa kutambua thamani
aliyokuwa nayo Yusufu kakuruhusu kufanya dhambi.tambua thamani yako hakika
hautachafua mwili na mawazo yako na hapo utafanikiwa.
·
Nini
hatima yako(destiny)
Kama
mwanafunzi na kiongozi ni muhimu sana kutambua hatima ya maisha yako ukiwa
shuleni na utakapotoka shuleni. Ni muhimu na itakusaidia sana utakapogundua
kuwa wewe ndiye mwenye maamuzi baada ya kuwa mwanafunzi,baada ya kuwa kiongozi
nini kitafuata baada ya hapo. Ninakuhakikishia kabisa ukishayatambua haya
maeneo itakubadili nautakuwa wa tofauti sana si katika masomo tu pia katika
maisha ya kila siku.
NB:Kumbuka kuwa katika maisha ya mwanadamu yeyote unayemwonalazima awe
ameyajibu maswali hayo hapo juu vizuri,nakushauri jaribu utaona mabadiliko
makubwa.
ITAENDELEA WIKI IJAYO USIKOSE
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon