jambo la msingi ambalo Mungu anataka ni kutembea na yeye, wapo watu katika ulimwengu huu wanaamini kabisa kwamba ni kwa mawazo yao au kwa akili zao wanaweza kupiga hatua.2kor 4:18 inasema tusiviangalie vinavyoonekana,kwa hiyo visivyoonekan(ulimwengu wa roho) ni muhimu sana kuliko vinavyoonekana. sababu ya kutumia mstari huu ni kukumbusha tu katika vitu visivyoonekana huwezi kutembea peke yako basipo Roho mtakatifu. Yesu alikuja hapa kwa kusudi moja tu kuutangaza ufalme wa mungu hata alipoondoka sawa na math 28:18-19 anasisitiza watu waliotembea nae kuwaeleza wengine ulimwenguni kuwa ufalme wa mungu umekaribia na kuwaelekeza njia hasa kiongozi wa msafara ambaye ni Yesu kristo pekee. ndugu ukiwa na kristo ndani yako hutataka wengine wapotee utatamani nao watembee na yeye. labda niseme hili jaribu kupima kiwango chako cha imani kwa kuangalia ni watu wangapi wamemjua kristo kupitia wewe. jambo lililofanyika msalabani ni kukuleta wewe kwa yesu halafu wewe uwalete wengine pia kwa Yesu na Yesu atatupeleka kwa baba hapo ndipo tunasema tunatembea na yesu.haleluyaah.
unapomjua yesu mambo yote yanakuwa safi,pia kumbuka vita hatupigani mwilini vinapiganwa rohoni hivyo kutokumjua Mungu kunaweza kukufanya usiijue nafasi yako ya kiroho.ndio maana watu unakuta mara sijui umenyolewa nywele au umeamka unaumwa bila sababu au kuonewa kwa namna yoyote tembea na bwana naye atakuongoza. nakutakia maisha mema katika kristo
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon