Ukiangalia mfumo wa maisha ulimwenguni unaonesha wazi kabisa kwamba wenye nguvu ndio wanaoweza kuitawala dunia. lakini katika uhalisia ni ngumu sana utakapogundua kuwa watu ambao tunawaona wana nguvu walishawahi kuwa dhaifu kabisa. iko mifano mingi ambayo ya mataifa na watu ambao kwakweli wanamajina lakini wametokea katika maisha duni kwa mfano Marekani ilikuwa nchi masikini kabisa,msanii wa filamu sylivester stalon(rambo),benn carson nawengine wengi maarufu unaowafahamu wana historia ambayo ukiambiwa utashangaa sana.
sehemu ya majengo ya chuo kikuu cha Dar es salam mahali ambapo watu huamini mabadiliko huanzia chuo. |
ukweli uliopo ni kwamba hao wote waliweza kuzika aina fulani ya maisha mengine pasipo kutafuta kiwango cha juu sana cha elimu ili waweze kufanikiwa.sio kwamba napinga elimu hapana lakini jambo muhimu ni kuzika aina ya maisha tunayoishi na kutamani sifa za majina yetu kusambaa kwa wengine hassa kwa kile tunachotakiwa kufanya.hivyo maisha yangu nayako yanategemea sana mtazamo sahihi ulio nao kuhusu maisha ya baadae. nasema hivi kufa tutakufa lakini tutamani kuacha kitu kitakacho tengeneza sifa ya jina lako lipate kuheshimiwa kwa yale mazuri utakayo yafanya mfano mzuri ni hayati mwalimu julius kambalage nyerere na mashujaa wengine Afrika na duniani kote.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon