Hakika mungu ni mwema karibu tena katika kipengele hiki ambacho kila jumatano huwa tunatazama mambo mbalimbali yanayohusu Tanzania kwa ujumla karibu tuendelee
Hali ya kijamii
Hali ya kijamii
Katika swala zima la kijamii kata ya bugabo pia kunashida kidogo kwani eneo hili ni kubwa sana ingawa swala la upatikanaji wa huduma za afya,maji na swala la miundombinu ya usafiri sio tatizo sana . changamoto kubwa ni katika elimu ambapo wanafunzi hujikuta wanatumia zaidi ya saa kwenda shule jambo ambalo huwa linamghalimu mwanafunzi muda kufika shule na kushiliki baadhi ya shughuli za nyumbani.hali inyopelekea watotowengi kuishia darasa la saba na kidato cha nne hali hii kwakweli haiwezi kuzaa matunda kwa kizazi kinacho jiita ni cha dijitali.utumikishwaji wa watoto wa shule za msingi kama kuleta kuni shuleni na kukata nyasi wakati wa saa za masomo umeonekana kama jambo la kawaida kwa wakazi wa bugaboo na wazazi wanaunga mkono kwa kuona kuwa inawapunguzia garama za kulipa shuleni.
Hali ya usalama pia sio nzuri kwani kipindi chote ambacho nimekaa bugabo hasa kitongoji cha bushasha nimishuhudia uchomaji hovyo wa nyasi katika uwanda unaozunguka eneo la ziwa Victoria na maeneo jirani pasipokuona hatua zozote za kuzuia tatizo hili kutoka serikalini na kwa wanakijiji kuzuia tukio hili pia hakuna elimu ya kutosha juu ya madhara yanayoweza kujitokeza endapo uchomaji huo utaendelea.hii hali inaondo dhamani ya ardhi ya mji huu ambayo kwakweli bado haijatumika na inafaa kwa kilimo cha zao lolote.serikali ya kijiji haiku karibu na wananchi wake kuhakikisha kuwa haki na usawa vinazingatiwa.
Hali ya kiuchumi
Mji wakagera kama nilivyotangulia kusema unafursa za kiuchumi nyingi sana ambazo ni hali ya hewa nzuri inayoruhusu kilimo cha mazao mbalimbali, vyanzo vya maji vya kutosha,ziwa Victoria,barabara zinazopitika,idadi kubwa ya watu n.k. pamoja na fursa zote hizi bado hali ya uchumi ni ngumu sana kutokana na wananchi hao kutokutumia fursa zilizopo kufanya uchumi ukue matokeo yake wana tegemea kilimo tu kujipatia kipato. Pia wananchi wa mji huu wameathiriwa sana na ulevi ambapo sio ajabu kukutana na mtu amelewa asubuhi. Katika mazungumzo na baadhi ya wauzaji wa pombe inaonyesha pia faida inayopatikana katika biashara hiyo ya pombe ni ndogo na haiwezi kukidhi mahitaji ya kusimamia familia.kutakona na hali ya ulevi imepelekea wakazi wake kuishi maisha duni sana yasiyo na tija.
Kagera imejisahau
Unaposema mji umetengwa na serikali ina maana hakuna huduma muhimu zinazohitajika kutolewa na serikali.mimi nasema kagera imejisahau yenyewe wala sio serikali kutokana na ukweli kwamba mji huu umeacha kumtumikia nakumwamini Mungu aliye hai ndio maana uko katika hali hiyo.wako wasomi wengi pia wahubiri na watu wanaomjua Mungu vizuri sana lakini hakuna jitihada za makusudi zinazochukuliwa kuikabili hali hii inamaanisha kwamba mji wao hauna dhamani.yote ambayo nimeonesha hapo juu wameshawahi kuyapitia na wanayajua hivyo kusema kwamba serikali imeisahau kagera ni matusi ila kagera imejisahau yenyewe. katika Nyanja za kijamii,kiroho na kiuchumi kuna watu ambao wanajua kabisa wajibu wao.muhimu kila mmoja lazima sasa asimame kwenye nafasi yake.mfano katika kitabu cha Nehemiah tunajifunza jinsi nehemia alichukua hatua kuhakikisha jerusalemu inajengwa,nehemia 2:2ff,3:1ff.Mtu mmoja anhitajika kuujenga kagera.
Maswala niliyojadili kama kuwepo kwa nguvu za giza,mfumo mbovu wa kijamii pamoja na kutokutumia rasilimali zilizopo sio tu ni la serikali ila kuna taasisisi na mashirika yasiyo ya uma yanayoweza kusimamia baadhi ya mambo.lakini kwa kusema haya si maanishi kwamba sertikari isiwajibike iwajibike katika maeneo yanayotakiwa kusimamia lakini maswala ya kiroho hayatatuliwi na serikali ila yanatatuliwa na watu wa rohoni waliosimama katika imani ya KRISTO hao ndio wenye suruhisho la kiroho.
MUNGU AKUBARIKI SANA.
Sign up here with your email
ConversionConversion EmoticonEmoticon