Tanzania yangu: Je tuko tayari kuchangia uchumi wa dunia?





Napenda nimshukuru Mungu kwa neema zinazoonekana kulifuata Taifa letu tangu tulipo azimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanzania bara. Katika safu hii leo naguswa kuuzungumzia uwekezaji mkubwa kuwahi kutokea afrika mashariki na barani Afrika kwa ujumla. Nazungumzia mpango wa taifa la Japan kuwekeza nchini Tanzania na kuifanya nchi yetu kuwa kitovu cha uchumi barani afrika .
Nimejaribu kuziita neema kwa kutazama upande mmoja lakini kwa ukweli tusipokuwa makini tunaweza kujikuta tumekuwa watumwa hasa kwa kutofaidika kwa kiasi kikubwa. Uwekezaji huu kwakweli umelenga kufanya jiji la Dar es salaam kuwa la kisasa zaidi. Jambo la muhimu hapa nikwamba kunamatokeo yanayoweza kutokea baada ya uwekezaji huo moja wapo ni ongezeko kubwa sana la watu mjini nahii inaweza kuongeza  hatari kubwa kwa wananchi.jambo la muhimu hapa  lazima hatua madhubuti zichukuliwe mapema kuhakikisha kuwa uwekezaji huo haugeuki janga kwa taifa.kwa mtazamo wangu jambo kubwa sana ambalo inabidi litazamwe kwa undani ni sera mbalimbali zinazohusu jamii hasa vijana kufanyiwa marekebisho au kutunga mpya ili ziweze kuendana na mabadiliko hayo.
Uwekezaji wa Japan nchini
Mapema mwishoni mwa wiki iliyopita ujumbe kutoka nchini Japani ukiongozwa na wazir anayehusika na maswala ya uchumi ulitua nchini . lengo kubwa likiwa ni kuleta ujumbe wa waziri mkuu wa Japani kwamba wameiteua Tanzania kuwa kitovu cha uchumi kwa nchi za afrika mashariki na Afrika kwa ujumla. Ambapo waliitaarifu serikali kuwa serikari hiyo itafanya uwekezaji nchini kwa kuanza kabisa waliweka makubaliano ya kuikarabati bandari ya Dar es salaam nakuifanya kuwa ya kisasa .ikiwa haitoshi pia wamewekamakubariano ya kuibadiri reli ya kati na kifanya iwe ya kimataifa zaidi. Pia makampuni makubwa Duniani ambayo ni Honda na Panasonic yakotayari kujenga viwanda hapa nchini ikiwa na maana kwamba bidhaa hizo zitazarishwa hapa nchini badala ya kuagizwa kutoka nje ya nchi.
Je tuko tayari?
Ukweli uliopo watanzania wengi nimejaribu kufanya utafiti mdogo tu kwa kuobserve kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii hatuko makini kufuatilia haya mambo. Hii inatokana najinsi tunavyojadili fursa mbalimbali tunazoweza kupata kutoka kwa wawekezaji waliomiminika kwa kipindi kifupi hasa mwezi july. Niwakati sasa wakuanza kutazama kwa usahihi na kuyatendea kazi yale yote ambayo tunadhani yatafaa. Naomba nitoe mfano ujio wa Barack obama raisi wa marekani ulizua maswali mengi na hoja ninazoziita za kipuuzi eti kwanini barabara zimesafishwa na hoja zingine nyingi ambazo kimsingi hazikuhusu ziara ya Obama. Jambo la msingi tujadili namna gani tutanufaika na ujio huo vinginevyo tutakuwa wateja wa mataifa yanayotuzunguka umiza kichwa wewe ambaye uko kazini , shuleni, vyuoni hata wajasiriamali namna gani utapata kunufaika wa wawekezaji hawa. Tuwe tayari kuumiza kichwa kwamba imetangazwa iko gesi mimi itanisaidia vipi kujikwamua na umasikini huu,Japani wanakuja na Mataifa mengi yatakuja kaa tayari Wewe mtanzania acha kushangaa. Tuilaumu serikali inapokosea lakini tusiwe vipofu kiasi hicho kutokutambua majira  na nyakati tulizonazo. Mimi naungalia uwekezaji huu kama kusimamia uchumi wa Dunia  hivyo natazama fursa hizi kwa level ya kimataifa je nafasi yangu itaendelea kuwa ya mtoto wa mkulima au nafasi ya mwekezaji katika uchumi wa Dunia?. Kazi kwako ndugu.


MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU BARIKI WATANZANIA.
Previous
Next Post »