Tanzania yangu

KAGERA MJI ULIOJISAHAU
Na Isack, Edward
Katika mambo yote namshukuru Mungu kwa nafasi ya pekee aliyonipa kufanya ziara ya kiuinjilist mkoani kagera.katika ziara yangu hii nimeweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo hali yakiroho, kijamiii na kiuchumi na kuweza kugundua mambo mbalimbali yanayopelekea mji wenye fursa nyingi kiasi hiki kushindwa kupenya katika maswala yote ya maendeleo kama ifuatavyo:-
Hali ya kiroho
Mkoa huu hauna hali nzuri ya kiroho ukilinganisha na mikoa kama Dar es salaam,Dodoma,mwanza na morogoro.sababu kubwa nilizo weza kuzihusisha na hali hii ya kiroho mkoani kagera ni pamoja na historia ya mji wenyewe ambao unaonekana kuwa kulikuwa na miliki kubwa sana na utawala wa nguvu za giza kwa mfano katika kata ya Bugabo ambayo iko katika wilaya ya bukoba ina zaidi ya vitongoji 20 baadhi yake ni  rushasha,katale,bushasha,rubafu,kyaka na maeneo mengine ambapo majina hayo yote ni majina ya mababu na mizimu iliyokuwa ikimiliki katika kipindi cha nyuma cha historia ya mji wa kagera katika maeneo hayo. hali hii imesababisha upofu wa kiroho katika huu mji kutokana mambo yafuatayo yanayoonyesha kuwa wamefungwa:-
Imani kwa mababu na mizimu, wakazi wa vitongoji hivi wanaamini sana katika mizimu kuwa ndio suruhisho la matatizo yao hivyo hutumia kila garama kuhakikisha wanaabudu mizimu ili kupata haja zao za kimwili na kiroho pia mfano baadhi ya wakazi huamini kuwa lazima kuwajengea mababu kijumba. kwa mujibu wa mwenyeji wangu ndugu benjamini yeye anasema kuwa huwa wana andaa vijumba hivyo ili kuwasiliana na mababu hao huku sauti ya babu husika aliyekufa muda mrefu husikika ndani ya kijumba hicho kinacho julikana kwa jina la nyaluju.hali hii imepofusha sana maisha ya watu wa kagera japo kuwa kwakweli ni mji wenye fursa nyingi sana za kiuchumi na kiroho pia hali inayopelekea wakazi wengi sana kujihusisha katika maswala ya kishirikina na kichawi.
Vifungo katika ufahamu, ukweli kabisa mji wa kagera kama ilivyo mikoa ya Dar es salaam unapoingia mjini utakutana na kundi kubwa la ombaomba, mji wa kagera wenyewe ni tofauti kidogo ukifika mjini utakutana na idadi kubwa ya watu wenye mtindio wa ubongo na matatizo mbalimbali ya akili. Hii inaashilia kwamba kunatatizo kubwa sana jambo ambalo linadhibitishwa na mwenyeji wangu ambaye yeye anadhibitisha kabisa kuwa katika eneo la bugabo watu huwa hawapendi mafanikio ya mtu mwingine jambo linalopelekea watu kutumia imani za kishilikina kufunga fahamu za watu. Hili ni tatizo kubwa sana katika huu mji hali inayopelekea kuto kuwepo kwa maendeleo yoyote.mfano mwingine katika vifungo vya ufahamu ni kijana Deus ambaye tulikutana nae eneo la Isaka wakati tukirudi kutoka kagera kijana huyu nae anaonekana kufungwa katika ufahamu wake baada ya baba yake kufariki ashukuriwe Mungu maana tulipomwombea alifunguliwa.katika hali hii ni ngumu sana kupata maendeleo katika mji huo.

sehemu ya mwambao  wa ziwa victoria mkoani kagera maarufu rwakajululuzi.
MUNGU AKUBARIKI
usikose sehemu inayofuata wiki ijayo.
Previous
Next Post »