UJANJAUJANJA KATIKA ELIMU CHANZO CHA MATOKEO MABOVU FORM4
katika yote namshukuru mwenyezi Mungu kwa kunipa uhai siku hii ya leo,kiukweli hii ni siku pekee kwangu.Nimenza kwa kichwa hicho cha habari nikitambua maumivu na huzuni karibu asilimia 60 ya familia za watanzania zinamajonzi juu ya matokeo ya kidato cha nne.ambapo kwa mujibu wa wazili wa elimu matokeo haya hayajawahi kutokea katika historia ya Tanzania.jambo ambalo si la kawaida.Haya yote ni matokeo ya ujanjaujanja tuu uliopo kuanzia kwa viongozi wetu mpaka kwa wazazi na wanafunzi husika,serikali imekuwa ikitoa sababu za kufanana tangu mwaka 2008 mpaka mwaka huu bila kuonesha hatua zilizochukuliwa huku bajeti ndogo sana ikiwekwa katka elimu huu mimi nauita ni ujanjaujanja maana hata pesa zinazotolewa hazifiki ndio maana utasikia waziri anakwambia uwiano wa vitabu eti kitabu kimoja kwa wanafunzi kumi does it make sense? .Hapana hii haikubaliki kabisa.Viongozi serikarini mi nawapongeza kwa ujanjaujanja wenu lakini nchi iko mikononimwenu itakapo twaliwa na aliyewapa hayo mamlaka ndio mtagundua kiasi gani yuko serious .
wazazi nao naona pia kama wajanja wajanja pia,mzazi makini huwezi ruhusu hali ya elimu kutokua na mwelekeo na mnakaa kutegemea serikali ninachofahamu huko mashuleni kuna kamati za wazazi je nini jukumu la wanakamati hao? huu ndio wakati wakupima mnachojadili kwenye hivyo vikao vyenu hakika sioni haja ya kamati za taaluma zisizo na tija pia mgundue kuwa sasa hatuhitaji majengo simamieni utoaji wa elimu.
wanafunzi kwa upande wao sisemi san lakini inapofikia mwanafunzi unaandika matusi na upuuzi kibao kwenye mtihani sijui unakua na akili gani.
swala la familia kumuandaa mtoto ki saikolojia ni kubwa sana wazazi kwakweli katika taifa hili ndio wakwanza kukwamisha maendeleo ya mtoto kwa kuwapa majina bandia kama,chizi,mjinga mpumbavu,mwendawazimu na majina mengine mengi na kauli za kukatisha tamaa ,hii haijengi hata kidogo. nidhahiri kabisa kuwa matokeo ya kidato cha nne ni matokeo ya ujanjaujanja wa wahusika katika tasnia ya elimu mpaka pale tutakapoamua kutumia akili zetu vizuri kuzalisha mawazo sahihi.
by.Isack,Edward
Sign up here with your email
1 comments:
Write commentsexactly
ReplyConversionConversion EmoticonEmoticon