HUKUANZA WEWE
katika mambo yanayokwamisha mtu kuweza kuendelea ni pale anapokutana na changamoto mbalimbali za maisha hasa pale unapokuta unashindwa kufikia malengo uliyoweka kwa wakati,hali hii moja kwa moja watu huweza kumlaumu Mungu.inawezekana umeshapitia magumu fulani na kama hujapitia basi jiandae maana lazima yaje hakuna namna unaweza kuzuia.wengi sana huwa wanaomba Mungu naomba nifanikishe katika jambo fulani.lakini sijawahi kusikia mtu akisema Mungu naomba jaribu hili ili nifanikiwe,hii ni sawa na mwanafunzi kutaka kupanda daraja la kimasomo pasipo kuomba mtihani.kiukweli ukikuta mwanafunzi ameomba mtihani ujue huyo mwanafunzi yuko vizuri sana.sio kwamba nasema tuombe majaribu lakini yanapotupata tusivunjike moyo maana kuna daraja ambalo Mungu anataka uvuke.hebu nikupe mifano hii :
daudi ilikuwa lazima ashindane na sauli ili awe mfalme,inawezekana hiyo haijakaa vizuri soma mdo 11:5-18 kwenye hii mistari kunamtihani mkubwa ambao petro anapewa yaani kuingia kwenye nyumba ya mtu asiye myahudi baada ya kushinda hili jaribu tunaona anafanikiwa kuingia kwa mtu wa mataifa,hapa ninachotaka kusema hapa nimashindano ambayo petro aliyapa wakati anapokea ujumbe,anakwenda kwa mtu yule na pia kwa wayahudi wenzake lazima walihoji kwamba wewe imekuwaje umeenda kwa mataifa,lakini ukifuatilia ushindi unakuja kupatikana pale wote wanapokuja kumtukuza Mungu.
ndugu yako mambo mengi na roho wa Mungu anawashuhudia wafanye jambo fulani matokeo yake mazingira yanawazuia kufanya yale ambayo Mungu anataka wafanye sikia changamoto hiyo hukuanza wewe ,hakikisha unayafanya yale tu ambayo Mungu amekupa kufanya.nahitimisha tu kwa msisitizo kwamba HUKUANZA WEWE BADIRIKA TIMIZA KUSUDI LA BWANA.
1 comments:
Write commentsAmen....
ReplyConversionConversion EmoticonEmoticon