Leo katika Historia ya kanisa la AICT lilikotoka kabla ya kuwa hivi 
lilivyo:Mnamo mwaka 1877-1909 lilikuwa likiitwa CMS yaani Church 
Missionary Society lilianza kazi ya kuhubiri Injili katika Afrika 
Mashariki,Bagamoyo Tanganyika,mwezi Julai 1876.Mwaka 1909-1937 Peter 
Cameron Scott  alianzisha AFRICA INLAND MISSION (AIM)mjini 
Philadelphia,USA.Madhumuni yake  ilikuwa ni kuhubiri Injili na kuanzisha
 makanisa katika bara la Afrika.Mwaka 1937-1956 kanisa kuanzishwa rasmi 
na kupewa jina la EKLEZIA EVANJELI YA 
KRISTO (E.E.K) nakupewa katiba iliyo wapa mamlaka na kanuni tatu zilizo 
andikwa katika katiba; 1.Kujitawala lenyewe 2.Kujitegemea lenyewe 
3.Kujieneza lenyewe.Wakati huu katiba ilikuwa imeandikwa kwa lugha ya 
Kisukuma na miniti zote za vikao. viliandikwa kwa Lugha hii.1957 Jina la
 kanisa EKLEZIA EVANJELU YA KRISTO lilibadirishwa na kuitwa AFRICA 
INLAND CHURCH TANGANYIKA Jina hili jipya liliandikwa katika 
katiba.Kujitawala halisi kwa A.I.C.Tanganyika kulipatikana 12/2/1960 
katika mkutano wa Synod na Field Council.Kwa wakati huo mkuu wa kanisa 
alikuwa akiitwa DIRECTOR yaani Mkurugenzi.Mkurugenzi wa kwanza  AICT ni 
Mch Jeremia Mahalu Kisula ambae baadae ndie aliyekuwa Askofu wa kwanza 
wa kanisa hili.Jina la Ukurugenzi lilibadirishwa na kuitwa Uaskofu mnamo
 mwaka 1966 na kuweza kuchaguliwa kila baaada ya miaka minne.Baadhi ya 
Majina ya  viongozi wa kanisa hili tangu mwanzo.1.Oneil .Luten Shergold 
2.Mch Alexander mckay.
SOURCE;Makongoro kwaya FB 
Sign up here with your email
 

3 comments
Write commentsNataka kua muumin
ReplyNiko Tabora
0765641246
MUNGU awabariki
ReplyAmeni
ReplyConversionConversion EmoticonEmoticon